Bustani kubwa zaidi ya mandhari ya barafu na theluji duniani yafunguliwa katika "mji wa barafu" wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2024
Bustani kubwa zaidi ya mandhari ya barafu na theluji duniani yafunguliwa katika
Watalii wakitembelea kwenye Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin, ambapo ni bustani kubwa zaidi ya mandhari ya barafu na theluji duniani, huko Harbin, mji mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang kaskazini mashariki mwa China, Desemba 21, 2024. (Xinhua/Yang Siqi)

HARBIN – Bustani kubwa zaidi ya mandhari ya barafu na theluji duniani, ambayo ni maonesho ya 26 ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin yamefunguliwa rasmi jana Jumapili saa 4 asubuhi huko Harbin, mji mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, ambao unajulikana pia kuwa ni "mji wa barafu na theluji."

Ikiwa na mada ya "Ndoto ya Majira ya baridi, Upendeleo wa Asia," bustani hiyo imejengwa kwa kutumia barafu na theluji zenye mita za ujazo 300,000, ikihusisha mambo yaliyochochewa na Michezo ijayo ya Majira ya Baridi ya Asia ya Harbin, ambayo itafunguliwa Februari mwaka ujao, mara tu baada ya likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

Michezo hiyo pia itakuwa mikubwa ya mashindano ya kwanza ya kimataifa ya michezo ya barafu na theluji kuandaliwa na China tangu Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing Mwaka 2022.

Bustani hiyo ni lenye eneo la mita za mraba jumla ya milioni 1, ukubwa wake umeongezwa kuliko ile ya mita za mraba 800,000 za mwaka jana, itakuwa bustani kubwa zaidi katika historia yake ya miaka 26.

Bustani hiyo ina sehemu tisa kubwa, miundo yake ni majengo ya barafu mbalimbali ambayo ni alama za miji ya nchi 42 na maeneo matatu ambavyo ni wanachama wa Baraza la Olimpiki la Asia (OCA), alama hizo ni kama vile Hekalu la Tiantan la Beijing China, Kasri la Osaka la Japani na Taj Mahal la India, majengo hayo ya Barafu yanaweza kung'alishwa kwa mwanga usiku.

Mnara mkuu umesimama kwenye mhimili mkuu wa bustani hiyo, ukiundwa kwa nguzo ndefu za barafu zinazoonyesha nembo rasmi ya OCA.

Saa moja tu baada ya bustani hiyo kufunguliwa, foleni ya watu kwenda Eneo la Kuteleza kwenye Theluji, Super Ice Slide ilitanda mamia ya mita.

"Ni bahati iliyoje! Leo ni siku ya mwisho ya safari yangu mjini Harbin, na sikutarajia kushuhudia ufunguzi wa Dunia ya Theluji na Barafu. Nina furaha sana kwamba ninahisi kama ninasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China mapema," amesema Dai Xiaoqin, mtalii kutoka Mji wa Wuhan wa Mkoa wa Hubei wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha