Mradi uliojengwa na kampuni ya China waleta maji safi kwa wanakijiji wa Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 24, 2024
Mradi uliojengwa na kampuni ya China waleta maji safi kwa wanakijiji wa Botswana
Picha hii iliyopigwa tarehe 15 Desemba 2024 ikionyesha sehemu ya mtambo wa kusafisha maji uliojengwa na Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China Tawi la Botswana mkoani Boteti, Botswana (Xinhua/Teng Junwei)

GABORONE – Siku moja asubuhi, mwandishi wetu wa habari alivumilia jua kali na kwenda nyumba ya Mmabaledi Tebalo, mkazi wa Kijiji cha Mokobaxane, katika Mkoa wa Boteti, kaskazini mwa Botswana.

Huku mama yake na kaka zake wakifurahia hali ya ubaridi kwenye kivuli cha mti, Tebalo mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akifungua bomba kwenye kona ya nyumba yake. Maji safi ya bomba yalikuwa yakitiririka. Tebalo kwanza aliosha uso wake na kisha kunywa maji moja kwa moja kwa kutumia kifundo cha kiganja cha mkono.

"Maji ya zamani yalikuwa na chumvi, lakini sasa ni matamu," amesema kwa msisimko.

Mradi wa kusambaza maji wa Boteli, Botswana uliojengwa na kampuni ya China

Boteti iko kaskazini mwa Botswana, ambayo ni umbali wa kilomita zaidi ya 100 kutoka Uwanda wa Chumvi wa Makgadikgadi kuelekea kaskazini, na karibu na Mgodi wa Almasi wa Orapa upande wa mashariki. Eneo hilo linakosekana na maji safi.

Wafanyakazi wa Shirika la Huduma za Maji la Botswana wanasema, maji ya ardhini katika eneo hilo yana chumvi nyingi na harufu mbaya, ambapo, yanapotumiwa kwa muda mrefu, yana madhara kwa afya. Kutokana na ukubwa wa eneo hilo na kutengana kwa wanakijiji, mradi wa usambazaji maji safi, ambao ulihitaji uwekezaji mkubwa, haukuwa umepewa kipaumbele hadi miaka ya hivi karibuni.

Mradi wa Usambazaji Maji wa Boteti ulianza kujengwa na Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China Tawi la Botswana Februari 13, 2023 na ulichukua muda wa miezi 18 kukamilika. Ulihusisha ujenzi wa miundombinu mikuu ya usambazaji maji na vifaa vingine, ikiwa ni pamoja na mabomba ya maji yenye urefu wa kilomita 184, pampu nne za nyongeza za kusukuma maji, matangi kumi ya maji yaliyoinuka, mabwawa matatu ya zege ya kuhifadhi maji, na muundo na ujenzi wa mtambo wa kutibu maji. Zaidi ya hayo, majengo mawili ya ofisi za utawala, nyumba kumi za wafanyakazi, na vifaa vingine vya umeme, mashine, na vifaa vya kuhisi kwa mbali vilijengwa.

Wanakijiji 30,000 kuwa wanufaika

Mradi huo wa kusambaza maji ulianza rasmi kufanya kazi Septemba mosi mwaka huu, jambo ambalo linawezesha watu wa kijiji hicho kupata maji safi ya bomba na hivyo kumaliza historia ya muda mrefu ya kunywa maji ya chumvi katika vijiji vinane vya mkoa huo kikiwemo Kijiji cha Mokobaxane. Wanakijiji takriban 30,000 wamefaidika na mradi huo.

Mmabaledi Tebalo amesema katika mahojiano na shirika la habari la China, Xinhua kuwa tangu kuzaliwa kwake amekuwa muda wote akitumia maji ya chumvi kwa kunywa, kupikia na kuoga. “Kutumia maji yenye chumvi kwa muda mrefu ni hatari kwa afya, lakini hatukuwa na namna nyingine,” amesema.

Bomgere Jane, mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Mokobaxane, amepongeza mradi huo wa usambazaji maji safi "Kampuni ya ujenzi ya China imetuletea mradi mzuri. Maji sasa ni safi, na maisha yamekuwa rahisi zaidi. Kila mtu kijijini anashukuru sana."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha