Wilaya ya China yabadilika kuwa vituo vya baiskeli za Watoto Duniani (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 25, 2024
Wilaya ya China yabadilika kuwa vituo vya baiskeli za Watoto Duniani
Tarehe 24, Oktoba, 2024, wafanyakazi wakiwa na pilikapilika za kazi kwenye mstari wa uzalishaji wa baiskeli za watoto katika Wilaya ya Pingxiang, Mkoa wa Hebei wa China. (Picha na Mu Yu/Xinhua)

Wakati sikukuu ya Krismasi ilipokaribia, bidhaa mbalimbali za baiskeli za watoto, baiskeli za watoto zinazotumia umeme, na vigari vya watoto wachanga vilikuwa vimeonekana kwenye rafu za maduka ya nchi mbalimbali na kwenye tovuti za maduka ya mtandaoni, zikiwa tayari kuuzwa kama zawadi kwa watoto.

“Vigari vyetu vya watoto wachanga, viti salama vya watoto kwenye magari vinauzwa katika Walmart na Amazon, na bidhaa zetu zote zinauzwa nje ya China, nyingi kati yao zinauzwa katika masoko ya Ulaya na ya Amerika ya Kaskazini,” alisema Qiao Xiaoguang, meneja mkuu wa kampuni ya Haohaizi tawi la Pinxiang Mkoani Hebei, China.

Kampuni ya Haohaizi ni moja kati ya wazalishaji 4,800 wa baiskeli za watoto, vigari vya watoto wachanga na magari ya kuchezea yanayotumia umeme huko Pingxiang. Katika miaka mingi iliyopita, wazalishaji hao wamekuwa wa kundi la viwanda katika Wilaya ya Pingxiang. Mwaka jana mapato ya kundi hilo yamezidi Yuan bilioni 30 (takriban Dola za Kimarekani bilioni 4.17).

Mnamo 2023, Pingxiang kwa jumla imezalisha baiskeli za watoto, vigari vya watoto wachanga na magari ya kuchezea yanayotumia umeme milioni 145, bidhaa hizo zimeuzwa katika nchi zaidi ya 80 kama vile Marekani, Russia, Ujerumani, na Kazakhstan. Wilaya hiyo iliyokuwa wilaya maskini ya China, baada ya kupata maendeleo makubwa ya viwanda vya baiskeli za watoto katika miaka 40 iliyopita, hivi sasa imekuwa kituo cha uzalishaji na utafiti wa baiskeli za watoto.

Saffir Chuniyan Kunnummal, mfanyabiashara wa India mwenye umri wa miaka 47 alisema, kampuni yake ya biashara za kimataifa imefikia makubaliano ya kushirikiana na kampuni za Pingxiang, na takriban makontena 20 ya baiskeli yanasafirishwa kutoka Pingxiang hadi soko la Dubai kila mwezi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha