Wakimbizi wa Syria wapata nyumba na matumaini nchini Misri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 26, 2024
Wakimbizi wa Syria wapata nyumba na matumaini nchini Misri
Wasyria wakifanya kazi kwenye mgahawa katika Mji wa 6th of October, ulioko karibu na Cairo, nchini Misri, Desemba 21,2024. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

Ahmed Enaba, Msyria na mpishi mzuri wa chakula cha Mashariki ya Kati Shawarma, alifungua ukurasa wake mpya nchini Misri mwaka 2016 akifungua mgahawa katika Mji wa 6th of October, sehemu yenye pilikapilika iliyoko karibu na Cairo.

Vitoweo vyake vimeunganisha ladha ya Wasyria na ukarimu wa Wamisri, vimependewa na wenyeji kwa haraka.

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Hayat Tahrir al-Sham umeendesha operesheni kubwa ya kijeshi kutoka kaskazini mwa Syria, Novemba 27. Walielekea upande wa kusini na kunyakua mji mkuu Damascus, na kupindua serikali ya Rais wa zamani wa Syria Bashar al-Assad ndani ya siku 12.

Kutokana na mabadiliko ya mamlaka ya hivi karibuni nchini Syria, Enaba alianza kuhisi mvuto wa maskani yake, Aleppo. Lakini mwanamume huyo wa makamo amekuza kwa kina maisha yake nchini Misri, ambayo anatunza sana. "Hapa ni nyumbani kwangu sasa. Nimejenga maisha na mustakabali wangu hapa," alisema.

Lakini, moyo wake unafikiria Syria, na anatumai siku ambayo anaweza kutoa mchango kwa ajili ya taifa lake kwa kufungua mgahawa wake mwingine huko Aleppo mara tu hali itakuwa salama zaidi.

"Ninataka kusaidia watu wangu kwa kuwatoa kazi na matumaini," Jose alisema.

Wakati Enaba alipofika Misri, alishangaa sana na ukarimu wa watu wa Misri, ambao walimpa eneo la hifadhi na maelekezo.

Eneba alikumbuka kuwa walinifanya nijisikie kama familia. Nilipata kazi kwa haraka, na kutokana na msaada wa jamii ya huko na huduma za serikali, niliweza kuanzisha mgahawa wangu."

Enaba alisema anathamini urafiki aliojengwa na wafanyakazi wenzake na wateja wa Misri. "Sitasahau kamwe mambo ambayo watu wa Misri wamenifanyia," alisema kwa dhati.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji linasema kuwa Misri ni nyumba kwa wahamiaji na wakimbizi milioni 9, wakiwemo Wasyria milioni 1.5.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha