China yadhamiria kutoa juhudi za kuongeza matumizi katika manunuzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2024
China yadhamiria kutoa juhudi za kuongeza matumizi katika manunuzi
Picha iliyopigwa Februari 2, 2024 ikionyesha mandhari ya Eneo la Great Tang mjini Xi'an, mji mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, kaskazini-magharibi mwa China. (Xinhua/Shao Rui)

BEIJING - Mkutano wa Kamati Kuu ya Kazi ya Uchumi ya China wa kuweka malengo ya kiuchumi ya mwaka mzima umedhamiria kuongeza matumizi katika manunuzi kwa nguvu, kuboresha ufanisi wa uwekezaji, na kupanua mahitaji ya wanunuzi wa ndani katika nyanja zote mwaka ujao.

Wakati China hapo awali ilikuwa ikitegemea uwekezaji na mauzo ya nje kwa upanuzi wa uchumi wake, matumizi kwenye manunuzi yamezidi kuchukua nafasi kubwa katika miaka ya hivi karibuni chini ya mkakati wake wa kuendeleza muundo wa maendeleo wa "mzunguko wa pande mbili", ambao unachukua soko la ndani kama mhimili mkuu huku ukiruhusu masoko ya ndani na ya kimataifa kuimarishana.

Katika robo tatu za kwanza za mwaka 2024, matumizi kwenye manunuzi yalichukua asilimia 49.9 katika ongezeko la uchumi wa China, yakipita kwa kiasi kikubwa uwekezaji na mauzo ya nje, ambavyo vilichukua asilimia 26.3 na 23.8, mtawalia.

Mtandao wa reli wa China ulipata idadi kubwa ya safari zilizovunja rekodi katika miezi 11 ya kwanza ya mwaka huu, kutokana na kuimarika kwa uchumi na kufufuka kwa sekta ya utalii.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli la China, sekta ya reli ilishughulikia safari za abiria zaidi ya bilioni 4 kuanzia Januari hadi Novemba, idadi ambayo ni mara ya kwanza kufikia kiwango hicho ndani ya mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa kituo cha takwimu cha Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China, katika robo tatu za kwanza za mwaka 2024, safari za watalii katika vijijini na maeneo ya pembezoni mwa miji ziliongezeka kwa asilimia 15.5 kwa mwaka hadi kufikia takriban bilioni 2.25, na mapato ya jumla yameongezeka kwa asilimia 9.8 mwaka hadi mwaka, na kufikia yuan trilioni 1.32.

Watu wanapenda kutalii maeneo ya jadi ya utamaduni, huku wengi wao wakimiminika kwenye maeneo ya kihistoria wakati wa likizo za mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha