Jengo la Mnara wa Kupigia Mishale wa Zhengyangmen mjini Beijing lafunguliwa tena kwa umma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2024
Jengo la Mnara wa Kupigia Mishale wa Zhengyangmen mjini Beijing lafunguliwa tena kwa umma
Watu wakitembelea maonyesho ndani ya jengo la Mnara wa Kale wa Kupigia Mishale wa Zhengyangmen mjini Beijing, Desemba 26, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

Jengo la Mnara wa Kale wa Kupigia Mishale wa Zhengyangmen lililoko kando ya mstari wa katikati wa Mji wa Beijing limekuwa na historia ndefu ya kuanzia Enzi ya Ming (1368-1644), jana Alhamisi limefunguliwa tena kwa umma.

Lango la Zhengyangmen liko kwenye sehemu ya mwisho ya kusini ya Uwanja wa Tian'anmen, lango hilo lina majengo mawili: jengo la lango la upande wa kaskazini na jengo la mnara wa kupiga mishale upande wa kusini. Lango hilo linaonyesha uzoefu wa jadi wa usimamizi wa miji ya China katika zama za kale.

Wakati wa Enzi za Ming na Qing (1368-1911), jengo la Mnara wa Kupigia Mishale wa Zhengyangmen lilikuwa sehemu moja ya miundo ya lango ambayo ilitumika kwa madhumuni ya kujihami na kufanya hafla. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha