Daraja refu zaidi la kuvuka bahari katika Mkoa wa Guangxi lazinduliwa rasmi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2024
Daraja refu zaidi la kuvuka bahari katika Mkoa wa Guangxi lazinduliwa rasmi
Picha hii iliyopigwa kwa droni Desemba 24, 2024 ikionyesha Daraja la Longmen la Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

NANNING - Daraja la Longmen, ambalo ni daraja refu zaidi la kuvuka baharini katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, limezinduliwa rasmi jana Jumapili, likipunguza muda wa usafiri kati ya Bandari ya Qinzhou na Bandari ya Fangchenggang kutoka saa 1.5 hadi dakika 25.

Serikali ya mkoa huo imesema kuwa, Daraja hilo la Longmen la Mji wa Qinzhou lina urefu wa kilomita takriban 7.6. Linafuata usanifu wa barabara mbili, njia sita, na kiwango cha juu cha barabara za mwendo kasi, na kasi ya kuendeshwa kwa gari imefikia kilomita 100 kwa saa.

Daraja hilo ni njia muhimu katika eneo la kiuchumi la Ghuba ya Beibu na linatarajiwa kusaidia maendeleo ya sifa bora ya eneo hilo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha