China yaonesha kwa mara ya kwanza mfano wa aina mpya za treni ya mwendo kasi zaidi duniani (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2024
China yaonesha kwa mara ya kwanza mfano wa aina mpya za treni ya mwendo kasi zaidi duniani
Picha hii ikionyesha mwonekano wa ndani ya behewa la daraja la kibiashara la treni ya mwendokasi ya CR450AF mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 29, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING – Mfano wa aina mpya za treni ya mwendokasi ya CR450, yenye kasi ya majaribio ya hadi kilomita 450 kwa saa na kasi ya uendeshaji ya kilomita 400 kwa saa, umeonyeshwa kwa mara ya kwanza mjini Beijing siku ya Jumapili, ikionyesha maendeleo yenye hali ya juu ya China katika teknolojia ya reli na mchango wake kwa sekta ya reli duniani.

Treni hiyo ya mwendokasi ya CR450 ina kasi zaidi kuliko treni za mwendokasi za CR400 za Fuxing zinazotoa huduma kwa sasa, ambazo zinaendeshwa kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa.

Kundi la Kampuni za Shirika la Reli la China litapanga mfululizo wa majaribio mbalimbali kwa aina hizo mpya za treni na kuboresha viwango vya kiufundi ili kuhakikisha treni hiyo ya CR450 inaingia kwenye huduma ya kibiashara mapema iwezekanavyo.

Kuendeshwa na uvumbuzi

Ikilinganishwa na treni tangulizi zake, ukinzani wa jumla wa uendeshaji wa treni hiyo ya CR450 utapungua kwa asilimia 22 na uzito wake utapunguzwa kwa asilimia 10, kundi hilo la kampuni za shirika la reli la China limesema

Mfano huo wa Aina mpya za treni ya mwendokasi ni modeli mbili za CR450: CR450AF na CR450BF, zote zikiwa na muundo wa mabehewa manane huku mabehewa manne yakiendeshwa na injini na mengine manne yasiyo na injini, kwa mujibu wa CRRC, muundaji mkuu wa treni nchini China.

Treni hizo za mwendokasi zina sifa ya mfumo wa hali ya juu, mfumo wa kupozwa kwa maji, mfumo wa kudumu wa kuvuta sumaku, na mfumo magurudumu wa kuaminika na wenye utulivu, ukihakikisha ufanisi bora na salama wakati wote wa uendeshaji.

Treni hizo zina mfumo wa hali ya juu, wa ngazi mbalimbali wa breki na vihisi zaidi ya 4,000 kwa ajili ya usimamizi wa wakati halisi wa mifumo muhimu, ikiwa ni pamoja na bodi la treni, pantografu yenye voltage ya juu, udhibiti wa treni na mifumo ya kutambua moto.

Ufikiaji duniani

Tangu ilipozindua reli ya kati ya miji ya Beijing na Tianjin mwaka 2008 yenye kasi ya kilomita 350 kwa saa, China imejenga mtandao mpana zaidi na wa hali ya juu zaidi wa reli ya mwendokasi duniani.

Miradi mikubwa kama vile Reli ya mwendokasi ya Guangzhou-Shenzhen-Hong Kong imeimarisha kwa kiasi kikubwa mawasiliano na maendeleo ya kikanda. Hadi sasa, urefu wa jumla wa njia za reli ya mwendokasi zinazofanya kazi nchini China umefikia kilomita takriban 47,000, kama inavyoonyeshwa na takwimu kutoka Mamlaka ya Taifa ya Reli ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha