Fuyang Anhui: Mavuno makubwa kwenye mabanda ya nyanya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2024
Fuyang Anhui: Mavuno makubwa kwenye mabanda ya nyanya
Wanachama wa Ushirika wa Upandaji Mboga katika eneo la Yingdong, mjini Fuyang, mkoani Anhui walichuma nyanya kwenye mabanda ya nyanya wakijiandaa kuzisafirisha hadi sokoni kwa ajili ya kuuzwa, Desemba 29, 2024.

Katika miaka ya hivi karibuni, eneo la Yingdong, mjini Fuyang limebadilisha muundo wake wa kilimo kulingana na hali ya eneo hilo na kutumia mfumo wa "ushirika + vituo + wakulima" ili kuwaongoza wakulima kupanda nyanya, biringani, matango na mboga nyingine za kijani zisizo na uchafuzi wa mazingira, kuongeza mapato ya wakulima na kusaidia ufufuaji wa vijijini kwa pande zote. (Picha na vip.people.com.cn)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha