

Lugha Nyingine
Uturuki yalenga kuvutia watalii wengi zaidi wa China Mwaka 2025, ikitangaza maeneo mapya ya vivutio
![]() |
Watalii wakitembelea mji wa kale wa Aizanoi katika Jimbo la Kutahya, Uturuki, Desemba 27, 2024. (Mustafa Kaya/ kupitia Xinhua) |
Uturuki inavutia idadi inayoongezeka ya watalii wa China kwenye maeneo maarufu ya vivutio kama vile Kapadokia, Pamukkale, na Efeso, huku pia ikitangaza maeneo ya utalii yasiyojulikana sana kama vile pwani ya Bahari Nyeusi.
Juhudi zinazoongozwa na Shirika la Kutangaza na Kuendeleza Utalii la Uturuki na mashirika ya usafiri wa watalii ya kikanda zinaendelea kutangaza maeneo mapya ya utalii, Irfan Karsli, mkuu wa Shirika la Utalii la Ligarba amesema.
Juhudi zinazopewa kipaumbele ni katika eneo la Mashariki ya Bahari Nyeusi, ambalo ni maarufu kwa vyakula vyake, magofu ya Kirumi, na mazingira mazuri ya asili.
"Mipango ambayo ni pamoja na kuandaa safari za kufahamiana kwa mashirika ya usafiri wa watalii ya China, kwa kujikita zaidi na Trabzon katika eneo la Bahari Nyeusi," Karsli amesema.
Fatma Sahin, meya wa mji wa kati wa mkoa wa Gaziantep kusini mashariki mwa Uturuki, pia ametangaza vyakula mbalimbali wa mji wake vinavyotambuliwa na UNESCO katika hafla iliyofanyika mapema mwezi huu.
Bertan Oner, Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni mwanzilishi wa Hotelz, shirika la kwanza la mtandaoni la usafiri wa watalii la Uturuki, amesisitiza namna kizazi cha Z nchini China kinavyohimiza wimbi jipya la watalii wenye shauku.
"Wanataka kujionea maeneo mapya waliyoyaona kwenye mitandao ya kijamii," Oneer ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.
Uturuki ilipokea watalii 381,200 wa China katika miezi 11 ya kwanza ya Mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 70.88 mwaka hadi mwaka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma