

Lugha Nyingine
Usafirishaji Gesi ya Russia kupitia Ukraine hadi Slovakia wasitishwa (2)
![]() |
Picha hii iliyopigwa Desemba 18, 2022 ikionyesha vifaa katika kiwanda cha kugeuza gesi kuwa kimiminika cha Kovykta mjini Irkutsk, Russia. (Xinhua/Meng Jing) |
BRATISLAVA – Usafirishaji gesi ya Russia kupitia Ukraine hadi Slovakia umesitishwa rasmi jana siku ya Jumatano, huku shirika kuu la usambazaji gesi nchini humo Slovakia, SPP likichukua hatua kuhakikisha kusambaza gesi asilia bila kusita.
Usafirishaji wa gesi ya Russia kupitia Ukraine umesitishwa katika eneo la kuingilia la Velke Kapusany kwenye mpaka wa Ukraine na Slovakia, shirika la kusambaza gesi la Slovakia, Eustream limetangaza kwenye tovuti yake.
Shirika la gesi la serikali ya nchi hiyo, SPP limesema siku hiyo hiyo kwamba litaendeleza usambazaji salama wa gesi asilia kwani limekuwa likifanya maandalizi kwa ajili ya usitishaji huo kwa muda mrefu, vyombo vya habari vya nchini humo vimesema.
Kwa mujibu wa SPP, shirika hilo limenunua gesi kutoka vyanzo visivyo vya Russia, kupaunua njia za usafirishaji gesi, na kuhakikisha gesi asilia ya sasa iliyohifadhiwa kwenye matangi kuongeza kwa asilimia 20 zaidi kuliko mwaka mmoja uliopita, Shirika la Habari la Jamhuri ya Slovakia limesema.
Eustream, kwa upande wake, limeweka wazi kuwa gesi asilia inasafirishwa katika maeneo yote ya viunganishi kwa mujibu wa mapendekezo ya wateja na imefanya maandalizi ya kutosha kutimiza wajibu wake kwa wateja na kuhakikisha usafirishaji.
SPP ilitoa taairfa kwa Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen sambamba na Eustream na kampuni zingine nchini Austria, Hungary, na Italia mapema mwezi huu, ikisema kwamba usafirishaji gesi kupitia eneo la Ukraine ni "suluhisho la faida zaidi siyo tu kwa watumiaji wa gesi wa Ulaya, lakini pia kwa Ukraine yenyewe."
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico pia alionya katika barua kwa Umoja wa Ulaya (EU) Desemba 29, 2024, kwamba kukubali kimya kimya uamuzi wa Ukraine wa kusitisha usafirishaji huo wa gesi ya Russia kutaongeza hali ya mvutano.
Waziri mkuu huyo wa Slovakia pia alielezea imani kwamba usitishaji huo wa usafirishaji gesi utadhuru EU zaidi kuliko Russia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma