Shughuli ya kubadilisha vyombo vya umeme vya zamani  kuwa vyombo vipya yahimiza matumizi mkoani Guangxi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2025
Shughuli ya kubadilisha vyombo vya umeme vya zamani  kuwa vyombo vipya yahimiza matumizi mkoani Guangxi
Wakazi wa mji wakichagua vyombo vya umeme nyumbani katika sehemu ya kuuza vyombo hivyo . (Picha na He Ning/People's Daily Online)

Jioni ya tarehe 31 Desemba, Shughuli ya Usiku wa kung'aa wa Biashara ya Vyombo vya Umeme ya Mwaka Mpya wa Njia Mpya ya Hariri ya Guangxi 2025 ilifanyika mjini Nanning, katika mkoa wa Guangxi. Katika shughuli hiyo, Soko la Mwaka Mpya la China (Guangxi)-ASEAN 2025 lilifunguliwa katika hali motomoto. Katika sehemu ya kubadilisha vyombo vya umeme nyumbani vya zamani kuwa vyombo vipya, hali mpya ya matumizi imeonekana wazi, wafanyabiashara na kampuni nyingi zimeanzisha shughuli ya punguzo kubwa la bei ya bidhaa Mwaka Mpya kwenye msingi wa ruzuku za serikali na kuvutia watu wengi kuuliza na kununua.

Habari zinasema kuwa , kuanzia mwisho wa Novemba hadi Desemba 31, Mkoa wa Guangxi ulianzisha shughuli ya Matumizi ya Majira ya Baridi ili kuhimiza ustawi wa soko la matumizi ya mwisho wa mwaka. Hadi sasa, idadi ya washiriki kwenye shughuli hiyo ya kubadilisha vyombo vya umeme nyumbani vya zamani kuwa vyombo vipya mkoani Guangxi imezidi milioni 4.09, na kwa jumla kuchochea thamani ya mauzo ya bidhaa husika kuzidi Yuan bilioni 26.2.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha