Madaktari wa China watoa huduma katika mstari wa mbele nchini Vanuatu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2025
Madaktari wa China watoa huduma katika mstari wa mbele nchini Vanuatu
Guo Ziyang, muuguzi wa chumba cha upasuaji wa timu ya madakari ya China, akiangalia vifaa vya upasuaji katika Vila Central, hospitali kuu ya Port Vila, Vanuatu, Januari 2, 2025. (Xinhua/Long Lei)

Wataalam wa kundi la tatu la timu ya madakati wa China nchini Vanuatu wametoa huduma za kitaalamu kwa wagonjwa zaidi ya 1,800 tangu walipowasili nchi hiyo ya Kisiwa cha Pasifiki mwezi Septemba mwaka 2024.

Pia wamefanya upasuaji zaidi ya 300 na mafunzo karibu 30.

Desemba 17, 2024, tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.3 kwenye kipimo cha richta lilipiga Port Vila, mji mkuu wa nchi hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya mji huo na vifo visivyopungua watu 14. Timu hiyo ya madaktari wa China, licha ya watu wake kupata majeraha katika tetemeko hilo, imekuwa timu ya madaktari wasio wenyeji ya kwanza kutoa huduma za dharura katika eneo lililoathirika zaidi na tetemeko hilo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha