Njia mbili za moja kwa moja za reli ya mwendokasi zaunganisha Mikoa ya Shaanxi na Hubei ya China Bara na Hong Kong (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2025
Njia mbili za moja kwa moja za reli ya mwendokasi zaunganisha Mikoa ya Shaanxi na Hubei ya China Bara na Hong Kong
Wafanyakazi wakifanya onyesho kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya treni ya mwendokasi kutoka Xi'an hadi Hong Kong kwenye Stesheni ya Reli ya Xi'an Kaskazini mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini-magharibi mwa China, Januari 5, 2025. (Xinhua/Li Yibo)

XI'AN/WUHAN - Huduma mpya za reli ya mwendokasi inayounganisha Hong Kong na Miji ya Xi'an na Wuhan, miji miwili mikubwa ya China, zimezinduliwa rasmi jana Jumapili, zikiimarisha kwa kiasi kikubwa mawasiliano kati ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong na China Bara.

Treni iliondoka kutoka Xi'an, mji mkuu wa Mkoa wa Shaanxi kaskazini-magharibi mwa China, saa 5:04 asubuhi (kwa saa za Beijing), na nyingine iliondoka Wuhan, mji mkuu wa Mkoa wa Hubei katikati mwa China, saa kumi jioni, huku stesheni zote mbili za kuondokea zikiandaa maonyesho na shughuli nyingine za kusherehekea.

Treni kati ya Hong Kong na Xi'an, pia inasimama stesheni Wuhan, safari moja katika pande zote mbili inachukua chini ya saa 11, huku stesheni nyingine zikiwa katika mikoa ya Shaanxi, Henan, Hubei, Hunan na Guangdong.

Treni zinazoondoka Wuhan hazichukui zaidi ya saa tano kufika Hong Kong, zikisimama katika mikoa ya Hunan na Guangdong. Treni za kurudi kwenye njia hiyo zimepangwa kuondoka Hong Kong saa 1:19 asubuhi, siku inayofuata.

"Ili kuhakikisha huduma za hali ya juu, tumewapa mafunzo wahudumu wetu kufahamu vyema kufanya kazi kwa kutumia lugha za Kikantoni na Kiingereza," amesema Luo Xin, naibu mkuu wa stesheni ya Xi’an chini ya Shirika la Kundi la Kampuni za Reli la China Tawi la Xi'an.

Kwa mujibu wa shirika hilo, kufunguliwa kwa njia hizo mbili mpya kunamaanisha kuwa safari nne za treni sasa zinafanya kazi kati ya Hong Kong na Wuhan, mji ambao una wakazi zaidi ya milioni 13, zikileta urahisi na ufanisi zaidi kwa abiria wanaosafiri kwa likizo, shughuli za kibiashara au safari za muda mfupi.

Hong Kong iliingia katika zama ya reli ya mwendokasi mwaka 2018, wakati sehemu ya Hong Kong ya Reli Unganishi ya Huduma za Haraka ya Guangzhou-Shenzhen-Hong Kong Express ilipofunguliwa.

China inalenga kupanua urefu wa njia zake za reli ya mwendokasi hadi kufikia kilomita takriban 60,000 ifikapo mwaka 2030, kutoka kilomita 48,000 zilizokuwepo hadi mwishoni mwa 2024, takwimu kutoka kwa waendeshaji wa reli ya nchi hiyo zinaonyesha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha