Mkuu wa idara ya usalama wa rais wa Korea Kusini aapa kuzuia kukamatwa kwa Yoon aliyeondolewa madarakani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2025
Mkuu wa idara ya usalama wa rais wa Korea Kusini aapa kuzuia kukamatwa kwa Yoon aliyeondolewa madarakani
Wafuasi wa Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Yoon Suk-yeol wakiwa wamekusanyika katika maandamano karibu na makazi ya rais mjini Seoul, Korea Kusini, Januari 5, 2025. (Picha na Jun Hyosang/Xinhua)

SEOUL - Mkuu wa idara ya usalama wa rais wa Korea Kusini, Park Jong-joon, ameapa kuendelea kuzuia jaribio la kumkamata Rais aliyeondolewa madarakani Yoon Suk-yeol, akisema kama idara hiyo ya usalama, ambayo inaweka kipaumbele chake katika usalama wa rais, itafuata utekelezaji wa amri hiyo ya kukamatwa kwa Yoon, itakuwa ni kutotimiza wajibu wake na kuachana na usalama wa rais.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumapili, Park amebainisha kuwa atakubali wajibu wowote wa kisheria kwa makosa yake yanayoweza kutokea katika uamuzi wake wa kuruhusu maofisa wa idara hiyo kukabiliana na kundi la wachunguzi waliovamia makazi ya rais katikati mwa Seoul siku ya Ijumaa ili kuendelea na utekelezaji wa amri ya kumtia nguvuni Yoon.

Baada ya uzuiaji huo wa haki kutendeka wa idara hiyo kusababisha kushindwa kwa jaribio la kumkamata Yoon, wimbi la shutuma limeibuka likiielezea idara hiyo ya usalama kutenda kama walinzi wa kibinafsi, huku hata wito ukitolewa kwamba idara hiyo ya usalama inapaswa kuvunjwa.

Muswada wa kumshitaki Yoon ulipitishwa katika Bunge la Korea Kusini Desemba 14 mwaka jana, na uliwasilishwa kwenye mahakama ya kikatiba ili kuijadili na kuitolea hukumu ya mwisho kwa hadi siku 180, ambapo katika kipindi chote hicho mamlaka ya urais ya Yoon yatakuwa yamesimamishwa.

Yoon, ambaye alitajwa na mashirika ya uchunguzi kama mshukiwa kiongozi wa mashtaka ya uasi, alitangaza amri ya sheria ya kutawala kijeshi usiku wa Desemba 3, lakini amri hiyo ilibatilishwa na Bunge saa chache baadaye.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha