China Yafanikiwa Kurusha Satelaiti ya Shijian-25

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 08, 2025
China Yafanikiwa Kurusha Satelaiti ya Shijian-25
(Picha na Du Xinxin/ Chinanews)

Saa 10:00 asubuhi, Januari 7(Saa za Beijing), China ilirusha kwa mafanikio satelaiti ya Shijian-25 kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Xichang, kwa kutumia roketi ya Long March-3B. Satelaiti hiyo iliingia kwenye obiti iliyopangwa kwa mafanikio, na jukumu la urushaji limefanikiwa kikamilifu.

Satelaiti ya Shijian-25 hasa ilitumiwa kwa majaribio ya teknolojia ya kuongeza mafuta ya satelaiti na kuongeza muda wa maisha ya satelaiti.

Hii ni safari ya 555 ya anga ya juu kwa roketi za mfululizo wa Long March.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha