

Lugha Nyingine
Uungaji mkono wa kisaikolojia watolewa kwa watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Xizang, China (5)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 13, 2025
Tan Xiren, mtaalam wa Taasisi ya Saikolojia katika Taasisi Kuu ya Sayansi ya China, na wataalam wengine wa timu ya uungaji mkono wa kisaikolojia siku ya Alhamisi wiki iliyopita walifika katika makazi mbalimbali ya muda katika Wilaya ya Dingri iliyokumbwa na tetemeko wa ardhi, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China.
Kwenye makazi ya muda ya watu katika Kijiji cha Cuoang, Tan aliandaa shughuli mbalimbali kwa watoto zaidi ya 80 ili kutoa uungaji mkono wa kisaikolojia kwao baada ya tetemeko la ardhi. Timu hiyo pia inapanga kutoa mafunzo kwa timu ya walimu wenyeji wa kutoa ushauri wa kisaikolojia, ili kuwapa huduma bora wakazi waliokumbwa na tetemeko hilo la ardhi.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma