Jumuiya ya Wachina nchini Zimbabwe yaadhimisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa Nyoka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 13, 2025
Jumuiya ya Wachina nchini Zimbabwe yaadhimisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa Nyoka
Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding akipaka rangi macho ya simba kwenye sherehe za Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China mjini Harare, Zimbabwe, Januari 11, 2025. (Xinhua/Xu Zheng)

HARARE - Jumuiya ya Wachina nchini Zimbabwe imesherehekea Mwaka mpya wa Jadi wa Nyoka siku ya Jumamosi kwa kufanya shughuli ya kitamaduni katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe mjini Harare, mji mkuu wa nchi hiyo ambapo wageni walifurahia maonyesho mbalimbali, yakiwemo ya muziki, ngoma, sanaa ya kupigana ya China na sarakasi yaliyowasilishwa na wasanii wa China na Zimbabwe, ikionyesha uhusiano wa kitamaduni kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyovutia idadi kubwa ya raia wa China wanaoishi nchini Zimbabwe, Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding amesema mwaka mpya wa jadi wa China unaojulikana pia kwa jina la Sikukuu ya Spring ni wakati wa kuungana kwa familia na kupeana upendo na baraka.

"China na Zimbabwe zinazingatia sana kuhifadhi mila na urithi wa kitamaduni, jambo ambalo naamini ni muhimu katika kutafuta ustawi. Katika kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili dunia ya leo, tunaweza na tunapaswa kupata hamasa, hekima na nguvu kutoka kwa tamaduni, mila na falsafa zetu za kale," Zhou amesema.

Akizungumzia maendeleo ya uhusiano kati ya China na Zimbabwe, Zhou amesema mwaka 2024 ni "mwaka wenye mavuno mengi" kwa ushirikiano wao, akiangazia kukamilika na kuanzishwa kwa miradi kadhaamikubwa, ambayo imetelekezwa kupitia uungaji mkono wa kifedha kutoka kwa serikali ya China na uwekezaji kutoka sekta binafsi.

"Tunaposherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China, tunasherehekea pia ushirikiano imara na mshikamano usioyumba kati ya China na Zimbabwe," Zhou ameongeza.

Tukio hilo pia lilitoa tamasha kubwa la kitamaduni kwa wenyeji, ambao walivutiwa na mambo ya jadi ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kupitia maonyesho na vyakula halisi vyenye asili ya China.

Wageni wengi walionyesha upendo wao juu ya utajiri na uchangamfu wa utamaduni wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCCO) limeiorodhesha "Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, desturi za kijamii za watu wa China katika kusherehekea mwaka mpya huo wa jadi" kwenye Orodha ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu.

Mwaka Mpya wa Jadi wa China utaangukia Januari 29 mwaka huu, ikianzisha Mwaka wa Nyoka. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha