Maonyesho ya mabaki ya kale ya kitamaduni ya Enzi ya Tang mkoani Shaanxi yaanza Tianjin, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2025
Maonyesho ya mabaki ya kale ya kitamaduni ya Enzi ya Tang mkoani Shaanxi yaanza Tianjin, China
Watembeleaji wakipiga picha ya sanaa ya ufinyanzi wa udongo ya rangi tatu inayometa, ambayo inaonyesha mpanda ngamia anayefuga mifugo na kuishi maisha ya kuhamahama, kwenye Jumba la Kitaifa la Makumbusho ya Mambo ya Bahari ya China mjini Tianjin kaskazini mwa China, Januari 15, 2025. (Xinhua/Sun Fanyue)

Maonyesho ya mabaki ya kale ya kitamaduni ya Enzi ya Tang ya China (618-907 AD) yanayohifadhiwa katika Mkoa wa Shaanxi, kaskazini mwa China yameanza jana Jumatano katika Jumba la Makumbusho ya Taifa ya Mambo ya Bahari ya China mjini Tianjin.

Maonyesho hayo yanaoneshwa vitu 120 hivi (vikiwemo pamoja na seti za vitu) vya mabaki ya kale ya kitamaduni kutoka taasisi nane za kitamaduni katika mkoa huo wa Shaanxi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha