Stempu za mwaka mpya wa nyoka zatolewa katika Taasisi ya Confucius mjini Minsk, Belarus

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2025
Stempu za mwaka mpya wa nyoka zatolewa katika Taasisi ya Confucius mjini Minsk, Belarus
Wafanyakazi wakionyesha kwa mara ya kwanza stempu za "Mwaka wa Nyoka" kutoka mfululizo wa "Kalenda ya Mashariki" mjini Minsk, Belarus, Januari 15, 2025. (Picha na Henadz Zhinkov/Xinhua)

MINSK – Stempu za "Mwaka wa Nyoka" kutoka mfululizo wa "Kalenda ya Mashariki" ambazo ni kwa ajili ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa kalenda ya kilimo ya China zimetolewa katika Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Serikali ya Belarus mjini Minsk jana Jumatano.

Seti ya stempu sita, yenye kichwa cha "Kalenda ya Mashariki: Mwaka wa Nyoka," inajumuisha picha ya nyoka katikati. Kona ya chini kulia ina neno la lugha ya Kichina la "Nyoka" pamoja na maneno "Mwaka wa Nyoka" yaliyoandikwa kwa lugha ya Kibelarusi.

Waziri wa Mawasiliano na Habari wa Belarus Konstantin Shulgan amesema uchapishaji wa stempu hizo unaonyesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni wa karibu namna gani.

Balozi wa China nchini Belarus Zhang Wenchuan amesema, utoaji wa stempu hizo za kalenda ya kilimo ya China nchini Belarus umekuwa tukio kubwa kwa China na Belarus kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa pamoja, ikisaidia kuongeza maelewano na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha