Mahakama ya Korea Kusini yakataa ombi la Rais Yoon la kuachiliwa huru

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2025
Mahakama ya Korea Kusini yakataa ombi la Rais Yoon la kuachiliwa huru
Picha hii ikionyesha mwonekano wa Jengo la Serikali la Gwacheon, ilipo Ofisi ya Uchunguzi wa Ufisadi kwa Maafisa wa Ngazi ya Juu (CIO), mjini Gwacheon, Korea Kusini, Januari 16, 2025. (Picha na Jun Hyosang/Xinhua)

SEOUL - Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Seoul nchini Korea Kusini imekataa ombi la Rais Yoon Suk-yeol aliyekamatwa la kuachiliwa huru jana Alhamisi, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vingi vya habari, ambapo mahakama hiyo imepitia uhalali wa kukamatwa kwa Yoon kutokana na ombi la wakili wake wa utetezi, ikikataa kulikubali kwa kuwa hakukuwa na "sababu" ya kuitisha upitiaji wa uhalali wa kisheria.

Wakili wa Yoon alidai kuwa Ofisi ya Uchunguzi wa Ufisadi kwa Maafisa wa ngazi ya Juu (CIO) haina mamlaka juu ya kesi ya Yoon huku hati ya kukamatwa kwake ikipaswa kutolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Seoul, na si Mahakama ya Wilaya ya Seoul Magharibi.

Yoon hakutokea katika kesi hiyo ya faragha kutokana na masuala ya kiusalama, lakini mawakili wake walimtetea kwa niaba yake.

Wakati wa upitiaji huo wa mahakama, muda wa kukamatwa kwa Yoon wa saa 48 ulikuwa bado ndani ya sheria kuanzia saa 8 mchana, kwa saa za Seol (0500 GMT) wakati kitengo cha uchunguzi wa pamoja kilipowasilisha nyaraka husika mahakamani.

Yoon alikamatwa katika makazi ya rais Jumatano wiki hii, na kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo aliyeko madarakani kukamatwa.

Baada ya kuhojiwa katika ofisi ya shirika hilo la kupambana na ufisadi mjini Gwacheon, umbali mdogo kusini mwa Seoul, Yoon aliwekwa kizuizini katika Kituo cha Kizuizi cha Seoul kilichoko Uiwang, umbali wa kilomita tano tu kutoka ofisi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha