Wanafunzi wa kigeni wawa watu wa kujitolea wa Stesheni ya Treni ya Lanzhou katika pilika za kuwahudumia wasifiri wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 20, 2025
Wanafunzi wa kigeni wawa watu wa kujitolea wa Stesheni ya Treni ya Lanzhou katika pilika za kuwahudumia wasifiri wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Wanafunzi wa kujitolea wa kigeni wakipiga picha na watoto katika Stesheni ya Reli ya Lanzhou Magharibi Januari 18, 2025. (Xinhua/Chen Bin)

Wakati wa pilika ya kuwahudumia wasafiri wengi ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China mwaka huu, wafanyakazi wenye shughuli nyingi katika Stesheni ya Reli ya Lanzhou Magharibi, Mkoa wa Gansu, kaskazini-magharibi mwa China, wameungana na timu ya wanafunzi wa kigeni wanaosaidia abiria kubeba mizigo, kusaidia ukaguzi wa usalama, na kutoa huduma za kujibu maulizo.

Timu ya wanafunzi hao wa kigeni wa kujitolea imeundwa na wanafunzi 10 kutoka nchi za Kenya, Chad, Laos, Afghanistan na Madagascar, ambao wanasoma katika Chuo Kikuu cha Lanzhou.

Wanafunzi hao wa kujitolea walioalikwa na idara ya reli, wamepewa fursa ya kuhisi hali halisi ya kipekee ya pilikapilika za kuwahudumia wasafiri wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

"Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China inakaribia kuwadia, nikiwa mtu wa kujitolea katika pilika za kusaidia abiria kurudi nyumbani kujumuika pamoja na familia, nafurahia uzoefu wangu huu wa kujivunia," Kalbe Brai Madoue, mwanafunzi kutoka Chad amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha