Wasanii Vijana wa China na bendi ya shule ya UN wafanya maonesho ya michezo ya sanaa New York kwa kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2025
Wasanii Vijana wa China na bendi ya shule ya UN wafanya maonesho ya michezo ya sanaa New York kwa kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Wanafunzi kutoka Kundi la Michezo ya Sanaa la Vijana la Jinfan la Beijing wakifanya maonesho ya michezo ya sanaa kwenye Kituo cha Lincoln mjini New York, Marekani, Januari 20, 2025. (Xinhua)

NEW YORK - Wanafunzi takriban 400 kutoka Kundi la Michezo ya Sanaa la Vijana la Jinfan la Beijing na Bendi ya Shule ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa Jumatatu usiku wa juzi Jumatatu walifanya pamoja maonesho ya michezo ya sanaa ya kuvutia kwenye Kituo cha Lincoln jijini New York, Marekani kwa kusherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ambayo inaangukia Januari 29 mwaka huu.

Maonesho hayo ya michezo ya sanaa yamefanyika kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Wu Tsai katika Jumba la David Geffen, likivutia hadhira ya watu zaidi ya 2,500, wakiwemo wakazi wenyeji na watu wa eneo la makazi ya Wamarekani wenye asili ya China.

Maonesho hayo ya michezo ya sanaa yameonesha hali ya muunganisho wa michezo ya jadi na ya hivi sasa, ya Mashariki na ya Magharibi, yakihusisha aina mbalimbali za michezo ya sanaa ikiwa ni pamoja na muziki wa jadi wa China, okestra ya simfoni, ala za kupulizwa, uimbaji wa kwaya, densi, ngoma, Oprea ya Beijing, na michezo ya Gong Fu.

Yolanda Keahey, mfanyakazi wa maktaba kutoka Mji wa Jersey, New Jersey, ambaye alitazama maoensho hayo ya michezo ya sanaa, ametoa maoni yake akisema: "Maonyesho ya wanafunzi yalikuwa ya kushangaza! Nimevutiwa sana na Okestra ya Jinfan Simfoni na kikundi cha ngoma, na mavazi ya kupendeza yameongeza sana hali ya mvuto kwa ujumla."

Fu Xianqing, mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya ya Hisani ya Sanjiang ya New York, ambaye alitazama maonesho hayo akiwa amevalia mavazi ya jadi ya Wachina, amesisitiza umuhimu wa mawasiliano ya kitamaduni na mawasiliano kati ya watu wa kawaida wakiwa kama daraja kati ya China na Marekani.

"Michezo ya Sanaa haina mipaka. Kila noti na kila hatua ya ngoma usiku wa leo inasimulia simulizi ya urafiki na matumaini," amesema.

Hu Xinyue, mmoja wa wanafunzi waliofanya maonensho ya michezo ya sanaa , ameeleza ushiriki wake binafsi: "Nyuma ya jukwaa, nilihisi woga na wasiwasi, lakini mara nilipopanda jukwaani, taa zenye kung'aa zilinipa hali ya kujiamini na nia moja, nilichangamana ndani kabisa, na maonyesho yalipomalizika , nilihisi fahari na furaha."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha