

Lugha Nyingine
Utalii wa dunia wakaribia kurudi katika kiwango cha kabla ya COVID mwaka 2024 (3)
![]() |
Picha hii iliyopigwa tarehe 27 Desemba 2022 ikionyesha mwonekano wa Guadalupe huko Extremadura, Hispania. (Picha na Gustavo Valiente/Xinhua) |
MADRID - Idadi ya watalii wanaosafiri nchi za nje iliongezeka kwa asilimia 11 katika kipindi cha mwaka 2024, na kufukia bilioni 1.4, Kipimajoto cha Utalii Duniani (World Tourism Barometer) kilichochapishwa na Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa jana Jumanne kimeonyesha.
Takwimu hizo, ambazo zimechapishwa katika siku ya kuamkia maonyesho ya kimataifa ya utalii ya FITUR mjini Madrid, Hispania zinamaanisha kuwa idadi hiyo ya watalii imerejea hadi kufikia asilimia 99 ya kiwango cha mwaka 2019 kabla ya janga la COVID-19.
Katibu Mkuu wa Shirika hilo Zurab Pololikashvili amepongeza matokeo hayo akisema: "Katika kipindi cha 2024, utalii duniani ulifufuka kutoka kwenye janga la COVID-19 na katika maeneo mengi watalii wanaowasili na hasa mapato tayari ni ya juu kuliko mwaka 2019."
Ukuaji unatarajiwa kuendelea katika kipindi cha mwaka 2025, amesema, "kutokana na mahitaji makubwa yanayosababisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya vivutio vya watalii vyote maarufu na vile vinavyoibukia."
Shirika hilo la utalii lenye makao makuu yake mjini Madrid limeripoti kuwa Asia na eneo la Pasifiki zimeshuhudia wasafiri wa kimataifa milioni 316 mwaka 2024, kiasi ambacho kimeongezeka kwa asilimia 33 (watu milioni 78) kuliko mwaka 2023, na asilimia 87 ya viwango vya kabla ya janga ya COVID-19.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma