China na Uholanzi zaahidi kujenga uchumi wa dunia wenye wazi, kuimarisha ushirikiano wa maendeleo ya kijani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2025
China na Uholanzi zaahidi kujenga uchumi wa dunia wenye wazi, kuimarisha ushirikiano wa maendeleo ya kijani
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Mfalme wa Uholanzi Willem-Alexander mjini The Hague, Uholanzi, Januari 22, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

HAGUE – Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang amekutana na viongozi wa Uholanzi siku za Jumatano na Alhamisi mjini The Hague ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kuhimiza uchumi wazi wa dunia, na kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kijani.

Ding, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alikutana kwa nyakati tofauti na Mfalme wa Uholanzi Willem-Alexander, Waziri Mkuu Dick Schoof, na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Tabianchi na Ukuaji wa Uchumi wa Kijani Sophie Hermans katika ziara yake ya siku mbili.

Ding amesema, chini ya uongozaji wa kimkakati wa viongozi wa nchi hizo mbili, uhusiano wa kiwenzi wenye wazi na kitendo halisi wa ushirikiano wa pande zote kati ya China na Uholanzi umekuwa ukiimarishwa mara kwa mara huku ushirikiano wenye mafanyikio makubwa katika nyanja mbalimbali, ukileta manufaa kwa nchi hizo mbili na watu wao.

"China ina nia ya kuimarisha zaidi mawasiliano na Uholanzi ili kuongeza hali ya kuaminiana, kuhimiza uhusiano wa pande mbili kupata maendeleo makubwa zaidi na kusaidia nchi hizo mbili kuharakisha kufikia malengo yao ya maendeleo," amesema.

Akisisitiza kwamba China na Uholanzi ni nchi zinazonufaika na zinazounga mkono uchumi wazi wa dunia, Ding amesema China ina dhamira ya kupata maendeleo yenye hali ya juu kupitia ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, ikikaribisha kampuni za Uholanzi kupanua ushirikiano na China.

"Inatarajiwa pia kuwa Uholanzi itaendelea kuweka mazingira ya biashara yaliyo ya haki, usawa na yasiyo ya kibaguzi kwa kampuni za China, kulinda maslahi ya pamoja na kudumisha minyororo ya uzalishaji na usambazaji duniani iliyo tulivu na isiyozuiliwa, na kutambua faida zinazowiana za pande hizo mbili, kunufaika kamoja fursa na kujiendeleza kwa pamoja,” Ding amesema.

Kwa upande wake Mfalme Willem-Alexander amesema kuwa Uholanzi inathamini hali ya kuaminiana na urafiki na inapenda kuzidisha ushirikiano na China ili kusukuma kwa pamoja maendeleo ya uhusiano kati ya Uholanzi na China.

"Katika kukabiliana na migogoro ya sasa ya siasa za kijiografia, nchi mbalimbali zinapaswa kuwasiliana kwa uwazi, kutafuta maoni ya pamoja, kushirikiana na kushughulikia kwa pamoja changamoto za dunia nzima," Mfalme ameongeza.

Naye Schoof amesema Uholanzi inahamasika na mafanikio ya maendeleo ya China na kuichukulia China kama mshirika thabiti, akiongeza kuwa Uholanzi inapenda kuimarisha mazungumzo na China, kuongeza maelewano na hali ya kuaminiana, na kupanua ushirikiano wa manufaa halisi katika sekta mbalimbali kama vile uhifadhi wa maji, maendeleo ya kijani na huduma ya matibabu na afya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha