

Lugha Nyingine
Kijiji mwanzilishi wa mageuzi ya vijijini ya China chaandika ukurasa mpya wa ustawi
![]() |
Wanakijiji wakionyesha bahasha nyekundu zilizo na gawio lao katika Kijiji cha Xiaogang cha Wilaya Fengyang, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Januari 25, 2025. (Xinhua/Huang Bohan) |
HEFEI - Siku chache tu kabla ya sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, wakaazi wa kijiji cha Xiaogang, kilichoko Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, wamekutana kwa furaha na kupata bahasha nyekundu zenye gawio la fedha.
"Familia yetu imepokea yuan zaidi ya 2,000 (dola za Kimarekani kama 279) mwaka huu, ambazo zinatosha kwetu kufanya manunuzi ya bidhaa za sikukuu," amesema mwanakijiji Yan Jinchang, mwenye umri wa miaka 82.
Hafla hiyo ya utoaji wa gawio imefanyika Jumamosi, na ikiwa imejaa msisimko. Kinyume na hali inayodhaniwa na watu kwamba vijiji vinakaliwa zaidi na wazee, kulikuwa na vijana wengi na watu wenye nguvu kwenye hafla hiyo -- wengi wao ni watu waliorejea kuishi kijijini wakiwa wamejawa na ndoto.
Baadhi ya vijana wamesimulia hadithi za Xiaogang na wageni, huku wengine wakifanya kazi kama watangazaji wa moja kwa moja mtandaoni wa hafla hiyo, wakiangazia mvuto wa kipekee wa kijiji hicho kupitia lenzi zao za kamera.
Licha ya kiasi kidogo, gawio hilo lililogawiwa katika Kijiji cha Xiaogang lina umuhimu mmkubwa katika hali ya jumla ya maendeleo ya vijijini ya China.
Kikiwa hapo awali kimekumbwa na ardhi isiyo rutuba na uhaba wa maji, Kijiji cha Xiaogang kilikuwa mahali ambapo wakaazi walitatizika kupata maisha. Hata hivyo, kila kitu kilibadilika mwaka 1978 wakati wakulima 18 walipobonyeza alama zao nyekundu za vidole kwa siri kuhusu makubaliano ya kumiliki ardhi ya pamoja kwa kaya binafsi.
Hatua hii ya kijasiri iliibua wimbi la shauku ya uzalishaji wa kilimo na kutoa msukumo mkubwa si tu kwa Xiaogang, bali pia kwa harakati pana za mageuzi na ustawishaji wa vijijini nchini China.
Jina la Kijiji cha Xiaogang tangu wakati huo limewekwa katika kumbukumbu ya taifa kama mwanzo wa mageuzi ya China, kikijipatia jina la "kijiji cha kwanza katika mageuzi ya vijijini" cha China
Juu ya msingi huu, Kijiji cha Xiaogang kimeendelea kuleta mageuzi katika sekta nyingi -- ikiwa ni pamoja na kodi na tozo za vijijini, haki za ardhi na umiliki wa pamoja wa mali.
Mwaka 2017, wanakijiji wote katika Kijiji cha Xiaogang waligeuzwa kuwa wanahisa wa jumuiya ya kijiji, ili kufaidika na maendeleo ya biashara kutoka kwa mali zisizoshikika za Xiaogang. Hadi sasa, jumla ya gawio lililotolewa kwa wanavijiji wa Xiaogang limezidi Yuan milioni 20.
Mwaka 2024, Xiaogang ilishuhudia faida zake zikipanda kwa mwaka wa saba mfululizo, huku utalii wa Kijiji hicho umetoa mchango mkubwa katika mafanikio hayo.
Shughuli mbalimbali za kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China zafanyika katika Nchi Nyingi
Muonekano wa Kisiwa cha Weizhou katika Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China
Hafla ya Kukaribisha Panda wa China yafanyika katika Bustani ya Wanyama ya Adelaide, Australia
Shughuli mbalimbali zafanyika sehemu mbalimbali China kukaribisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma