

Lugha Nyingine
Kampuni ya reli ya Afrika yaanzisha mpango wa matengenezo ya mabehewa na injini za treni za abiria
![]() |
Wafanyakazi wa matengenezo wakitazama sehemu za injini ya treni kwenye karakana ya matengenezo ya Reli ya Mombasa-Nairobi jijini Nairobi, Kenya, Januari 23, 2025. (Xinhua/Wang Guansen) |
Reli ya Mombasa-Nairobi ilizinduliwa mwezi Mei, 2017, urefu wake ulifikia kilomita takriban 480, inaunganisha jiji kubwa Mombasa la pwani ya Bahari ya Hindi na jiji kubwa Nairobi, mji mkuu wa nchi hiyo. Reli hiyo ni reli ya kwanza ya kisasa nchini Kenya tangu nchi hiyo ipate uhuru na inasifiwa kuwa mradi bora chini ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kati ya China na Kenya.
Baada ya miaka minane ya uendeshaji, Kampuni ya Uendeshaji wa Reli ya Africa Star (Afristar), kampuni inayoendesha Reli hiyo ya Mombasa-Nairobi, ilianzisha mpango wa matengenezo ya mabehewa 41 ya abiria na injini 10 Januari 15 mwaka huu. Huku ikiwa na mipango ya kukamilisha matengenezo hayo ifikapo Mei 31, majukumu haya yatapunguza mushkeli kwa injini za treni wakati wa uendeshaji na kuhakikisha usafiri endelevu na salama kwa wateja wake.
Shughuli mbalimbali za kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China zafanyika katika Nchi Nyingi
Muonekano wa Kisiwa cha Weizhou katika Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China
Hafla ya Kukaribisha Panda wa China yafanyika katika Bustani ya Wanyama ya Adelaide, Australia
Shughuli mbalimbali zafanyika sehemu mbalimbali China kukaribisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma