Uwanja wa Ndege Mjini Beijing washuhudia wasafiri wengi wanaoingia katika siku ya kuamkia Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2025
Uwanja wa Ndege Mjini Beijing washuhudia wasafiri wengi wanaoingia katika siku ya kuamkia Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Familia mchanganyiko wa raia wa kigeni na Mchina ikipiga picha kwenye eneo la uhamiaji katika kituo cha tatu cha kuondokea na kuwasili ndege cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, mjini Beijing, China, Januari 28, 2025. (Xinhua/Chen Zhonghao)

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, mjini Beijing, China ulishuhudia wasafiri wengi wanaoingia siku ya Jumanne, ambayo ilikuwa siku ya kuamkia Mwaka Mpya wa Jadi wa China. Wakati ambapo familia nyingi za Wachina zimerudi nyumbani kusherehekea sikukuu hiyo, raia baadhi wa kigeni wamechukua fursa ya sera za msamaha wa visa ya kuingia China au kusubiria kuunganisha ndege kwenda nchi nyingine kujionea na kufurahia hali ya sikukuu hiyo katika mji mkuu huo wa China. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha