Watalii wa kigeni wafurahia kutalii Mji wa Beijing, China wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 01, 2025
Watalii wa kigeni wafurahia kutalii Mji wa Beijing, China wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Maxime (wa kwanza kushoto) na Liza, watalii kutoka Uswisi, wakionyesha kitu cha ukumbusho walichonunua katika maonyesho ya hekalu sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China katika Bustani ya Ditan mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 29, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)

Wakati watu wa China wakisherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, idadi kubwa ya watalii wa kigeni wamekuja katika nchi hiyo kujionea na kushiriki utamaduni wa China kufuatia utekelezaji wa sera mpya ya watu wa kigeni kuingia China kwa muda.

China iliendelea kulegeza sera zake za visa mwaka 2024 ili kuongeza ufunguaji mlango na mabadilishano kati ya watu na watu, na kuruhusu wasafiri na wafanyabiashara wengi zaidi wa kigeni kutembelea nchi hiyo bila visa. Hatua yake ya hivi karibuni ni kurefusha muda wa sera hiyo ya abiria wa kigeni kuwepo nchini China bila visa, ambayo imeruhusu wasafiri stahiki wa kigeni kuwepo nchini humo kwa saa 240 bila visa.

Mwaka Mpya wa Jadi wa China unahusisha jadi za kijamii za watu wa China katika kusherehekea mwaka mpya wa jadi, na uliongezwa na UNESCO katika orodha yake ya urithi wa utamaduni usioshikika Desemba mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha