Bandari katika Mji wa Haikou wa China zahakikisha usafirishaji wenye ufanisi wa mazao bichi ya kilimo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2025
Bandari katika Mji wa Haikou wa China zahakikisha usafirishaji wenye ufanisi wa mazao bichi ya kilimo
Lori lililopakia mazao bichi ya kilimo likipandishwa kwenye meli katika Bandari ya Xinhai mjini Haikou, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Februari 3, 2025. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

Mlango-Bahari wa Qiongzhou mjini Haikou, Mkoani Hainan, kusini mwa China umeingia katika kilele cha wimbi la wasafiri wengi wanaorejea katika Mwaka Mpya wa Jadi wa China. Ili kuhakikisha kusafirisha mazao bichi ya kilimo kwa ufanisi, Bandari za Xinhai na Xiuying mjiini humo zimetekeleza mfumo wa kutenga nafasi maalum kwa ajili ya kupandishwa vizuri kwa magari ya usafirishaji. Madereva wanaweza kununua na kukaguliwa tiketi zao bila kushuka kwenye magari yao. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha