

Lugha Nyingine
Eneo la kimataifa la mapumziko ya Michezo ya Kuteleza kwenye Theluji la Mlima Jiangjunshan wa Xinjiang, China lastawi chini ya timu ya inayoongozwa na vijana
Likiwa linapatikana katikati ya Mji wa Altay, Eneo la Kimataifa la Mapumziko ya Michezo ya Kuteleza kwenye Theluji la Mlima Jiangjunshan wa Xinjiang, China ni eneo la utalii wa michezo ya kuteleza kwenye theluji milimani la ngazi ya 5S ya kitaifa. Likijulikana kwa theluji nyingi na msimu mrefu wa theluji, eneo hilo limekuwa kivutio kwa wapenda michezo ya kuteleza kwenye theluji na watalii walio na shauku ya kupata msisimko wa michezo ya majira ya baridi.
Eneo hilo linajivunia njia za kuteleza kwenye theluji zenye urefu wa jumla ya kilomita 70, ili kukidhi mahitaji ya wateleza kwenye theluji.
Usanifu, ujenzi na ukarabati wa kila siku wa eneo hilo unatekelezwa na timu inayoongozwa na kijana mwenyeji Qiao Mu. Kwa uungwaji mkono na eneo hilo la mapumziko la Jiangjunshan na kupitia uzoefu wa kazi wa miaka sita hadi saba, timu hiyo ya Qiao imeanzisha falsafa yao ya kujenga eneo hilo la mapumziko inayoendana na mahitaji ya sasa ya soko la michezo hiyo.
Kwa Qiao Mu, kujenga sehemu ya kuruka na vifaa vingine ni kutoa jukwaa tu kwa watelezaji kwenye theluji. Ili kuboresha jukwaa hilo, timu yake mara kwa mara hupanga mafunzo ya bila malipo na mashindano ya kuruka ya kujiburudisha kwa watelezaji kwenye theluji. “Katika eneo la michezo hiyo ya kuteleza kwenye theluji, siyo tu tunashindana na vikomo vya uwezo wa miili yetu, bali pia kufuata utamaduni wa uhuru na furaha katika kuteleza kwenye theluji,” amesema Qiao Mu.
Kwa mujibu wa takwimu za Idara ya Utalii na Utamaduni ya Altay, tangu mwanzo wa msimu wa kuteleza kwenye theluji wa 2024-2025 hadi Februari 1 mwaka huu, eneo hilo limepokea watalii zaidi ya 600,000, ikifikia ongezeko la 23% ikilinganishwa na mwaka uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma