Yingge, ngoma ya asili yenye umaarufu mkubwa katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 06, 2025
Yingge, ngoma ya asili yenye umaarufu mkubwa katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China
Wasanii wa kikundi cha kucheza ngoma ya Yingge wakionekana pichani mjini Shantou, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Februari 2, 2025. (Yao Jun/Xinhua)

Ngoma ya Yingge, au "ngoma ya wimbo wa shujaa," ni aina ya ngoma maarufu ya jadi katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. Ngoma hiyo hujumuisha pamoja opera, ngoma, na karate na iliorodheshwa kuwa kundi la kwanza la urithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa mwaka 2006. Ikiwa na historia ya kuanzia Enzi ya Ming (1368-1644), ngoma hiyo ya kijadi mara nyingi inachezwa wakati wa sikukuu za kijadi za China.

Ngoma hiyo imekuwa ikifuatiliwa sana kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii katika kipindi cha miaka miwili iliyopita huku video za ngoma hiyo zikikusanya mamilioni ya watazamaji mtandaoni.

Mwaka huu, vikundi vya kucheza ngoma hiyo ya Yingge kutoka Shantou mkoani Guangdong pia vimealikwa kufanya maonyesho kwenye majukwaa kadhaa ya ng'ambo kwa sherehe za Mwaka Mpya wa Jadi wa China. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha