

Lugha Nyingine
Mauzo ya “Magari ya Chongqing” katika soko la kimataifa yaanza kwa mwanzo mzuri katika mwaka mpya wa jadi (3)
![]() |
Magari yakisubiri kupakiwa kwenye treni katika stesheni ya reli ya Yuzui Chongqing, China, tarehe 6, Februari. |
Jana Alhamisi, Februari 6, treni ya JSQ (treni maalumu kwa ajili ya kusafirisha magari kamili) iliyokuwa imebeba magari 281 ya “kuzalishwa mjini Chongqing” imeondoka kwenye stesheni ya reli ya Yuzui mjini Chongqing, China.
Takwimu kutoka Kituo cha Uchukuzi wa Bidhaa wa Reli cha Chongqing zimeonesha kuwa katika kipindi cha likizo ya siku nane ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Shirika la Reli, Tawi la Chongqing limesafirisha jumla ya “magari ya Chongqing” 5,743, miongoni mwake, 1,807 yalikuwa magari kamili.
Imeripotiwa kuwa, wakati wa likizo hiyo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, treni zilizokuwa zimebeba magari kamili ya “kuzalishwa mjini Chongqing” zilikuwa zikiondoka kwenye stesheni ya reli ya Yuzui kila siku, zikitumia Njia Mpya ya Magharibi ya Nchi Kavu-Bahari na Reli ya China-Ulaya kwenda kwenye masoko ya Asia Kusini Mashariki na Ulaya.
Takwimu zilizotolewa na Forodha ya Chongqing hivi karibuni zimeonesha kuwa mji huo umeuza magari kamili 477,000 nchi za nje mnamo mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la 29.6% kuliko mwaka uliopita.
Picha na Tang Yi/Xinhua
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma