Maisha ya kawaida yarejeshwa katika maeneo ya makazi mapya mkoani Xizang baada ya tetemeko ya ardhi (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2025
Maisha ya kawaida yarejeshwa katika maeneo ya makazi mapya mkoani Xizang baada ya tetemeko ya ardhi
Watu wa kujitolea wakiandika maneno ya kutakia heri na baraka ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye karatasi nyekundu yanayobandikwa kwenye makazi ya muda katika Kijiji cha Gyiru, Wilaya ya Lnaze ya Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China, Januari 26, 2025. (Xinhua/Jigme Dorje)

Mwanzoni mwa mwezi Januari, tetemeko la ardhi la ukubwa wa 6.8 lilitokea katika Wilaya ya Dingri ya Mji wa Xigaze, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China, likisababisha vifo vya watu 126 na kubomolewa kwa maelfu ya nyumba. Wilaya nyingi za karibu, ikiwemo ya Lnaze, pia ziliathiriwa.

Hatua mfululizo za kuokoa maafa na kutoa msaada zimekuwa zikifanywa kwa kasi katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko hilo. Maisha ya watu yamerudi katika hali ya kawaida katika maeneo ya makazi mapya ikiwa ni pamoja na makazi ya muda, utoaji wa maji na umeme, vilevile upatikanaji wa huduma za simu na mtandao wa intaneti. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha