

Lugha Nyingine
"Jukumu la Kudumu" la Mtaalam wa China kuendeleza ardhi yenye rutuba na uzalishaji katika jangwa la Mauritania (3)
![]() |
Zhang Hong'en, mkurugenzi wa Kituo cha Kielelezo cha Mifugo nchini Mauritania, akilisha ng’ombe katika kijiji cha Idini nchini Mauritania, Januari 18, 2025. (Xinhua/Si Yuan) |
NOUAKCHOTT - Wakati wa likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China iliyomalizika mapema wiki hii, Zhang Hong'en na wenzake walibaki mbali na nyumbani, wakidhamiria kikamilifu kwa kazi yao katika Kituo cha Kielelezo cha Mifugo nchini Mauritania, kituo ambacho kinahifadhi ng'ombe karibu 400, wakati huohuo mashamba ya majaribio ya nyasi ya Juncao na alfalfa yakihitaji uangalizi wa kila wakati.
Kutoka Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania, barabara kuu ya jangwa inaelekea hadi kijiji cha Idini, ambako kituo hicho kinapatikana. Baada ya kuingia, mazingira magumu ya mchanga ghafla yanaondolewa kwa mandhari yaliyojaa ustawi. Chemchemi inapatikana katikati ya mzunguko wa makutano ya barabara, huku barabara pana za saruji zikielekea katika pande mbalimbali. Tausi wakitembea kwa raha na kobe wanasonga kwa mwendo wautakao wenyewe.
Asilimia zaidi ya 80 ya eneo la Mauritania limefunikwa na jangwa. Joto kali, ukame, rutuba duni ya udongo, na dhoruba kali za mchanga hufanya iwe vigumu sana kwa mimea kukuza. Zhang alipofika Mauritania kwa mara ya kwanza mwaka 2011, alidhamiria kugeuza ardhi hiyo kame kuwa ardhi yenye rutuba.
Mwaka 2017, ushirikiano wa kiufundi unaoungwa mkono na China kwa Kituo cha Kielelezo cha Mifugo ulizinduliwa rasmi katika kijiji hicho cha Idini. Leo, eneo hilo limekuwa "maskani ya pili" kwa Zhang na wenzake wanne, wakati huo huo Mauritania imekuwa "nchi yao ya pili."
Kwa miaka mingi iliyopita, wataalam hao wa China wamefaulu kuingiza alfalfa na kupanua kilimo chake kikubwa, ikisaidia kupunguza uhaba wa malisho ya mifugo kwa wenyeji. Kutokana na hayo, aina nyingi za mimea ya malisho sasa zimekita mizizi katika Jangwa la Sahara. Kati ya mwaka 2020 na 2024, timu hiyo ya wataalam imeendeleza ardhi ya jangwa yenye ukubwa wa hekta takriban 20 kwa majaribio ya upandaji malisho ya mifugo.
Mwezi Oktoba 2023, Zhang alipeleka mbegu za nyasi za Juncao nchini Mauritania kutoka kwenye shamba katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia nchini China. Alifanya majaribio linganishi juu ya umwagiliaji, kurutubisha, umbali kati ya mimea, na vigezo vingine ili kuanzisha mbinu ya kilimo iliyo mwafaka kwa hali ya hewa ya eneo hilo.
"Alfalfa hustawi kwenye hali ya hewa baridi, wakati Juncao inastahimili joto. Mimea hii miwili inaendana kikamilifu katika hali ya hewanchini Mauritania, ikihakikisha upatikanaji wa malisho ya ng'ombe na kondoo kwa mwaka mzima," ameelezea.
Amir Abdou, mkulima wa mifugo kutoka Idini, amekumbushia wakati ambapo kijiji chake kilikuwa kimezungukwa na eneo lisilofaa kwa uzalishaji na lenye mchanga, "Kondoo wetu ama walikufa kwa njaa au walibaki dhaifu," amesema.
"Shukrani kwa wataalam wa China waliotufundisha jinsi ya kulima Juncao na mimea mingine, hatimaye tuna malisho ya kutosha kulisha mifugo yetu. Leo, ninafuga kondoo kumi, wote wakiwa na afya bora. Asanteni, marafiki zangu wa China!" mkulima huyo ameeleza kwa hisia.
Kituo hicho cha kielelezo hakijikiti tu katika kulima mimea ya malisho iliyo mwafaka kwa tabianchi ya Mauritania lakini pia kinashirikiana na kampuni kutoka China kuchagua na kuzaliana ng'ombe wanaostahimili. Mbinu na matokeo hayo yatanufaisha kwa upana maeneo muhimu ya ufugaji mifugo kote nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma