Dereva wa treni ya mwendokasi ashuhudia maendeleo ya miundombinu ya usafiri ya maskani yake (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 11, 2025
Dereva wa treni ya mwendokasi ashuhudia maendeleo ya miundombinu ya usafiri ya maskani yake
Lu Jinsheng akirekebisha sare yake kabla ya kuanza kazi yake katika karakana ya treni ya mwendo kasi mjini Guiyang, Mkoani Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Februari 7, 2025. (Xinhua/Yang Wenbin)

Lu Jinsheng, dereva kijana wa treni ya mwendokasi kwenye reli kati ya Guiyang na Nanning nchini China, alizaliwa na kukulia kwenye Tarafa ya Yundong katika Mji wa Duyun, ambayo inapatikana kwenye njia hiyo ya treni ya mwendokasi.

Tangu kuzinduliwa kwa njia hiyo ya reli ya mwendokasi kati ya Guiyang na Nanning mwaka 2023, Lu amekuwa akiendesha treni za mwendokasi zilizosanifiwa kuwa na kasi ya kilomita 350 kwa saa, kupitia milima mikubwa na mahandaki marefu ya mikoa ya Guizhou na Guangxi. Kazi yake hiyo si tu inatoa chaguo la usafiri wa haraka kwa wakazi kando ya reli hiyo lakini pia huleta watalii wengi katika maskani yake.

Kutoka kuwa mvulana wa kijijini hadi dereva wa treni ya mwendo kasi, Lu ameshuhudia mageuzi makubwa ya miundombinu ya usafiri ya maskani yake, kutoka njia za matope na barabara za saruji hadi barabara kuu na reli za mwendo kasi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha