Onesho la “Wulong Xuhua” lafanyika kusherehekea Sikukuu ya Taa za Jadi ya China mkoani Guizhou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 13, 2025
Onesho la “Wulong Xuhua” lafanyika kusherehekea Sikukuu ya Taa za Jadi ya China mkoani Guizhou
Watu wakishiriki onesho la “Wulong Xuhua” kusherehekea Sikukuu ya Taa za Jadi ya China katika Wilaya ya Taijiang, Mkoa wa Guizhou, Kusini Magharibi mwa China, Februari 11, 2025. (Xinhua/Tao Liang)

Onesho la kijadi la "Wulong Xuhua" ni aina ya ngoma ya kijadi ya dragoni ya kabila la Wamiao la China inayotumbuizwa katikati ya fashifashi za fataki. "Wulong" inamaanisha ngoma ya dragoni, na"Xuhua" inarejelea fashifashi za kipekee za kienyeji.

Timu zaidi ya 100 za ngoma ya dragoni zimekusanyika katika Wilaya ya Taijiang kusherehekea Sikukuu ya Taa za Jadi ya China, siku ya 15 ya mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo ya China, ambayo iliangukia Februari 12 mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha