

Lugha Nyingine
Watu wa makabila mbalimbali washiriki kwenye shughuli ya Shehuo kusherehekea Sikukuu ya Taa ya Jadi ya China (5)
![]() |
Picha ikionyesha maonyesho ya michezo ya sanaa ya shughuli ya Shehuo ya Sikukuu ya Taa ya Jadi ya China huko Urumqi, China. (Picha na Hanting/People’s Daily Online) |
Tarehe 12, Februari, siku ya 15 ya mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo ya China, ambayo ni Sikukuu ya Taa ya Jadi ya China, maonyesho ya michezo ya sanaa ya shughuli ya Shehuo ya Sikukuu ya Taa ya Jadi ya China yalifanyika kwenye Kituo cha Utamaduni cha Urumqi. Kwenye maonyesho hayo, timu 16 za wachezaji wazuri kutoka Urumqi, pamoja na timu 4 zilizoalikwa maalum kutoka nje ya Xinjiang, ikiwa ni pamoja na mikoa ya Shaanxi, Anhui, Shanxi na Ningxia, wachezaji wa kila timu walionesha mtindo wake kipekee katika maonesho ya michezo yao ya sanaa na kuwapatia uhondo wa utamaduni watu wa makabila mbalimbali.
Habari zinasema kwamba, shughuli ya Shehuo ikiwa shughuli yenye umaalumu wa mila na desturi za Urumqi, maonesho yake ya mwaka huu yamekuwa makubwa, timu nyingi zimeshiriki kwenye shughuli na kufanya maonyesho mengi ya michezo ya sanaa ya kufurahisha. Shughuli hiyo inafuata mila na desturi za Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, na kufanyika kwa njia inayounganisha mila na desturi hizo na mitindo ya hivi sasa, miji na vijiji ili kurithisha na kukuza utamaduni wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China na kufungamanisha kwa kina shughuli za utamaduni na utalii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma