Mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika wahimiza maendeleo ya bara katika Kikao cha Baraza la Utendaji la AU (2)

(CRI Online) Februari 14, 2025
Mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika wahimiza maendeleo ya bara katika Kikao cha Baraza la Utendaji la AU
Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat (wa kwanza kulia) akihutubia kikao cha 46 cha kawaida cha Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU huko Addis Ababa, Ethiopia, Februari 12, 2025. (Xinhua/Michael Tewelde)

Kikao cha Kawaida cha 46 cha Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika (AU) kilianza Jumatano katika makao makuu ya AU huko Addis Ababa, Ethiopia, kikisisitiza haja ya haraka ya kuimarisha juhudi zinazolenga kukuza maendeleo ya bara hilo, utulivu na umoja.

Mkutano huo wa siku mbili, unaohudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje kutoka wanachama wa AU, unafanyika chini ya kaulimbiu ya AU ya mwaka 2025: "Haki kwa Waafrika na Watu Wenye Asili ya Afrika Kupitia Fidia."

Akihutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat alisisitiza umuhimu wa juhudi za pamoja ili kukuza amani na usalama katika bara zima. Alisisitiza umuhimu wa kustawisha utawala bora, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, ufadhili endelevu, na mageuzi ya kitaasisi ya AU. Pia alisisitiza haja ya kuimarisha nafasi na umoja wa Afrika katika jukwaa la kimataifa.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kinatazamiwa kuwachagua makamishna sita wa Kamisheni ya AU. Zaidi ya hayo, kitapitia mswada wa ajenda na maamuzi ya Mkutano wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU, ambao umepangwa kufanyika Februari 15 na16.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha