Habari Picha: Kituo cha Matengenezo yote ya Ndege katika sehemu moja mjini Haikou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 18, 2025
Habari Picha: Kituo cha Matengenezo yote ya Ndege katika sehemu moja mjini Haikou, China
Wafanyakazi wakiondoa rangi ya mwanzo ya ndege iliyoingia nchini China kutoka nje katika Kituo cha Matengenezo yote ya Ndege katika sehemu moja cha Bandari ya Biashara Huria ya Hainan mjini Haikou, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Februari 17, 2025. (Xinhua/Zhang Liyun)

Tangu Kituo cha Matengenezo yote ya Ndege katika sehemu moja cha Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, China kilipoanza kufanya kazi mwaka 2022, jumla ya ndege 83 na injini 17 zimetengenezwa na kukarabatiwa kwenye eneo hilo la forodha, zikiwa na thamani ya jumla ya Yuan bilioni 45.05 (karibia dola za Marekani bilioni 6.2).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha