Timu ya madaktari ya China yatoa huduma za matibabu na mafunzo nchini Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 18, 2025
Timu ya madaktari ya China yatoa huduma za matibabu na mafunzo nchini Ethiopia
Daktari wa China Li Hao, daktari wa kundi la 25 la timu ya madaktari wa China nchini Ethiopia, akichunguza upataji nafuu wa mgonjwa baada ya upasuaji akiwa na wahudumu wa afya wenyeji katika wodi ya Hospitali Kuu ya Beijing Tirunesh mjini Addis Ababa, Ethiopia, Februari 14, 2025. (Xinhua/Han Xu)

Kundi la 25 la timu ya madaktari wa China nchini Ethiopia liliwasili nchini humo Mei 2024 na limetoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wenyeji na mafunzo kwa madaktari wa nchini humo. Hospitali kuu ya Beijing Tirunesh ambayo madaktari hao wanafanya kazi ya kutoa huduma pia ilijengwa kama sehemu ya juhudi za muda mrefu za msaada wa serikali ya China kwa sekta ya Afya ya Ethiopia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha