Dunhuang katika Mkoa wa Gansu wa China  yakaribisha maendeleo mapya (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 19, 2025
Dunhuang katika Mkoa wa Gansu wa China  yakaribisha maendeleo mapya
Watalii wakitembelea Mapango ya Mogao huko Dunhuang, Mkoa wa Gansu, kaskazini-magharibi mwa, Juni 7, 2024. (Xinhua/Lang Bingbing)

Katika miaka 2,000 iliyopita, Dunhuang ilikuwa kituo muhimu kwenye Njia ya kale ya Hariri, ambapo Hariri na chai za China zilipitia lango hilo kuelekea nchi nyingine, huku bidhaa za kilimo kama vile zabibu, karoti na makomamanga zikiingia China.

Dunhuang inajulikana kwa mandhari yake ya kuvutia na umuhimu wa kihistoria, na ina hazina ya mabaki ya kale ya Dini ya Kibudha na vitu vya sanaa. Katika miaka ya hivi karibuni, Dunhuang imekuwa ikitumia ipasavyo rasilimali zake za utalii wa kitamaduni na imefanya juhudi kubwa za kuwavutia watalii na wasomi kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao wana shauku kubwa ya kufanya utafiti juu ya umuhimu wake wa kihistoria na kushuhudia uhuishaji wa utamaduni wake katika zama za hivi sasa.

Dunhuang ilikuwa sehemu ya makutano ya Mashariki na Magharibi kwenye Njia ya kale ya Hariri katika zama za kale na imekuwa na historia ndefu ya maelfu ya miaka, hivi sasa Dunhuang imehuishwa na imekuwa na sura mpya na inakaribisha maendeleo mapya. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha