

Lugha Nyingine
Mjumbe wa Bunge la China na mchomeleaji vyuma mstadi anayejitoa kwa mafunzo ya mafundi vijana (2)
![]() |
Sun Jingnan (wa pili kushoto) akizungumza na wafanyakazi wenzake katika karakana ya CRRC Tawi la Nanjing Puzhen, Mkoa wa Jiangsu wa China, mashariki, Februari 20, 2025. (Xinhua/Li Bo) |
NANJING - Sun Jingnan amekuwa akifanya kazi kama mchomeleaji vyuma katika Kampuni ya Vifaa vya Reli ya CRRC ya China Tawi la Nanjing kwa zaidi ya miongo mitatu, na pia shahidi wa maendeleo ya haraka ya sekta ya usafiri wa reli ya China.
Akiwa amekua kutoka fundi kijana hadi kuwa mtaalamu, Sun ni mshauri na mlezi kitaaluma kwa vijana wengi wenye vipaji katika sekta hiyo ya reli.
Anaamini kwamba fundi katika kazi yoyote ya ufundi anapaswa kuwa mwangalifu sana juu ya kila kitu anachofanya katika kazi yake, ili kufikia mafanikio wezekana.
Sun akiwa mjumbe wa Bunge la Umma la China, anafuatilia zaidi ujenzi wa njia za reli, elimu ya ufundi stadi, na utengenezaji kwa teknolojia za kisasa. Atatoa maoni na mapendekezo juu ya kuwaandaa wafanyakazi wenye ujuzi na maendeleo ya hali ya juu ya viwanda vya utengenezaji wa vifaa katika mkutano ujao wa tatu wa Bunge la 14.
“Mafundi ni jiwe la msingi na nguzo za ujenzi wa taifa la China,” Sun amesema, akitumai kuwa vijana wengi wenye vipaji watajiunga na kundi hilo la mafundi ili kurithisha moyo wa mafundi wastadi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma