Miundombinu ya eneo la vivutio vya utalii yasaidia kupunguza muda wa usafiri wa watoto kwenda shuleni mkoani Yunnan (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2025
Miundombinu ya eneo la vivutio vya utalii yasaidia kupunguza muda wa usafiri wa watoto kwenda shuleni mkoani Yunnan
Picha ya droni iliyopigwa Februari 23, 2025 ikionyesha lifti ya kutalii na mfumo wa gari la kebo katika eneo la vivutio vya utalii kwenye Mto Nizhu katika Tarafa ya Puli, Mji wa Xuanwei, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua/Jiang Wenyao)

Feburuari 23 ilikuwa siku ya muhula mpya kwa wanafunzi kwenda Shule ya Msingi ya Guanzhaiwan katika Tarafa ya Puli mkoani Yunnan, China. Watoto kutoka Kijiji cha Nizhuhe walifungasha mabegi yao na kuanza kwenda shuleni. Kinachowatofautisha na wanafunzi wengine ni namna ya usafiri wao.

Kijiji cha Nizhuhe ni kijiji kidogo kilichoko kwenye bonde lenye kina kirefu lililozungukwa kwa nusu na Mto Nizhu nchini China. Zamani, njia fupi zaidi ya wanakijiji kutoka kwenye makazi yao bondeni hadi juu ya mlima ilikuwa njia hatari ya miamba, na muda wa usafiri uliwachukua saa karibu sita kwenda na kurudi. Watoto na wazazi wao wanaoishi katika kijiji hicho walilazimika kufanya usafiri huo mgumu angalau mara moja kila baada ya siku kumi.

Mwaka 2022, mabadiliko makubwa yalitokea kwenye usafiri huo wenye changamoto. Eneo la vivutio vya utalii kando ya Mto Nizhu lilikamilisha ujenzi wake mpya na kuanza kufanya kazi. Lifti yenye urefu wa mita 268, magari ya kutazama mandhari na mfumo wa magari kwenye kebo vilianza kutumika, vikiwapa utumiaji wa bila malipo wanakijiji wa Nizhuhe na maeneo ya karibu. Hiyo safari ya kwenda shuleni ya watoto hao imekuwa "usafiri wa mawinguni".

Siku hizi, shukrani kwa magari, lifti na kebo za watalii za eneo hilo la vivutio vya utalii, muda wa usafiri wa watoto kwenda shuleni umepunguzwa kuwa nusu saa tu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha