Sekta binafsi ya Mji wa Chongqing, China yastawi kwa uungaji mkono wa sera

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2025
Sekta binafsi ya Mji wa Chongqing, China yastawi kwa uungaji mkono wa sera
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye mstari wa uzalishaji wa Kampuni ya Utengenezaji Mashine ya Chongqing Hwasdan katika Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, Februari 22, 2025.(Xinhua/Wang Quanchao)

CHONGQING -Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Chongqing imekuwa ikizindua sera mbalimbali za kuhimiza maendeleo yenye sifa bora juu ya sekta binafsi ya Mji huo, kusini magharibi mwa China, zikijikita katika maeneo kama vile uvumbuzi wa kiteknolojia, upanuzi wa soko na uungaji mkono wa kifedha. Mwaka 2024, thamani ya kiuchumi iliyoongezwa ya sekta binafsi ya mji huo wa Chongqing ilifikia yuan trilioni 1.98 (dola za Kimarekani karibu bilioni 273).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha