

Lugha Nyingine
Bustani ya ndani kubwa zaidi duniani ya mandhari ya barafu na theluji yafunguliwa tena Harbin, China (7)
Bustani ya ndani kubwa zaidi duniani ya mandhari ya barafu na theluji ambayo ni kivutio cha utalii kwenye eneo la “Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin”, imefunguliwa tena jana Alhamisi asubuhi baada ya bustani ya nje ya "Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin" kufunga rasmi shughuli zake za mwaka wa 26 siku ya Jumatano.
Kikiwa kinachukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 23,000, kivutio hicho cha watalii cha ndani cha mandhari ya barafu-na-theluji kimepitia maboresho na ukarabati wa aina mbalimbali.
Ikiwa ilizinduliwa awali Julai 2024, bustani hiyo ina vyombo vya kisasa vya kutazama na kusikiliza, sanamu za barafu zinazovutia, na baadhi ya mambo kutoka shughuli za miaka ya nyuma za bustani hiyo na Michezo ya Majira ya Baridi ya Asia Mwaka 2025.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma