Jumba la Makumbusho ya vitu vya kale lafunguliwa kwenye uwanja wa ndege Mjini Xian, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2025
Jumba la Makumbusho ya vitu vya kale lafunguliwa kwenye uwanja wa ndege Mjini Xian, China
Watu wakitembelea jumba la makumbusho ya mabaki ya kale ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Xi'an Xianyang mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini-magharibi mwa China, Februari 26, 2025. (Xinhua/Shao Rui)

XI'AN - Jumba la makumbusho linaloonyesha vitu vya kale vya kitamaduni ambavyo vilifukuliwa wakati wa awamu tofauti za ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Xianyang wa Xi'an, kituo kikubwa zaidi cha usafiri wa anga kaskazini-magharibi mwa China, limefunguliwa kwa umma kwenye uwanja huo juzi Jumatano.

Jumba hilo la makumbusho linachukua eneo lenye jumla ya ukubwa wa mita za mraba 6,400 na linaonyesha vitu vya kale vya kitamaduni vyenye historia inayoanzia vipindi kadhaa vya kihistoria katika zama za kale za China, amesema Hou Chao, meneja wa idara ya shughuli za kitamaduni katika Kundi la Kampuni za Maendeleo ya Biashara la Uwanja wa Ndege wa Magharibi mwa China (Xi'an).

"Katika siku zijazo, jumba la makumbusho litaboresha usanifu wake wa maonyesho na kuunganisha teknolojia za hali ya juu, likijumuisha vionyeshi vya AR na VR," Hou ameongeza.

Kuanzia Juni 2020 hadi Oktoba 2022, wakati wa upanuzi wa awamu ya tatu wa uwanja huo wa ndege, vitu vya kale ya kitamaduni 6,848 yalipatikana.

Vitu hivi ni pamoja na makaburi ya kale 4,093 na sehemu 2,755 za mabaki ya kale kama vile tanuru za kufinyanga udongo, mashimo ya majivu, kingo na barabara, na vitu zaidi ya 22,000 vilichimbuliwa.

Mji wa Xi'an ni kivutio maarufu cha watalii nchini China ambacho kinajivunia urithi mkubwa. Ukiwa ni maskani ya wapiganaji maarufu wa Terracotta na maeneo mengine mengi ya kihistoria kama Giant Wild Goose Pagoda na Bell Tower, mji huo wa Xi'an ulianzishwa miaka zaidi ya 3,100 iliyopita na uliwahi kutumika kama mji mkuu wa enzi 13 za China ya kale. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha