Teknolojia za kidijitali za kisasa zawezesha kituo cha zamani cha viwanda Kaskazini Mashariki mwa China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2025
Teknolojia za kidijitali za kisasa zawezesha kituo cha zamani cha viwanda Kaskazini Mashariki mwa China
Mfanyakazi akiendesha mashine za kusaga zinazodhibitiwa kidijitali kwenye karakana ya Kampuni ya Harbin Turbine mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Februari 26, 2025. (Xinhua/Wang Song)

HARBIN - Kama moja ya vituo vya zamani vya viwanda vya China, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China umekuwa ukitumia teknolojia za kidijitali za Akili Mnemba (AI) na teknolojia nyingine za hali ya juu ili kuzijenga upya sekta zake za kijadi za viwanda katika miaka ya hivi karibuni.

Shirika la Mambo ya Umeme la Harbin ni miongoni mwa viwanda vinavyowezesha maendeleo ya kiwango cha juu, vyenye ufanisi na endelevu kupitia teknolojia za kidijitali za AI.

Kutokana na miundo hiyo ya biashara iliyoboreshwa, Kampuni za Mashine za Umme ya Harbin, Harbin Turbine na ile ya Harbin Boiler zote hizo zikiwa ni kampuni tanzu za Shirika la Mambo ya Umeme la Harbin, zimeshuhudia thamani ya uzalishaji wa mwaka ikiongezeka kwa asilimia 19.22, asilimia 49.21 na asilimia 56.7, mtawalia, mwaka 2024.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha