

Lugha Nyingine
Meneja kijana atafuta uvumbuzi katika shughuli za kijadi za fataki za fashifashi (3)
Li Shijie alizaliwa mwaka 1996 katika familia inayojishughulisha na utengenezaji wa fataki za fashifashi kwa vizazi vingi. Wakati wa masomo ya Li nje ya nchi, fataki zenye kutoa fashifashi za kustaajabisha alizoshuhudia katika shughuli mbalimbali si kama tu ziliingiza na kukuza hisia yake ya kujivunia , bali pia ziliamsha ufikiriaji wake zaidi juu ya uboreshaji wa maonyesho ya fashifashi kwa nguvu za kisayansi na kiteknolojia.
Li alirudi kwenye maskani yake na kuwa meneja wa Kundi la Kampuni za Fataki za Fashifashi la Zhongzhou mwaka 2022. Mwaka mmoja baadaye, Li alianzisha Kampuni ya Teknolojia za Utamaduni ya Hunan Chizi na akaanza kufanya utafiti kuhusu mfano wa maonyesho ya 3D unaojumuisha droni na fataki baridi za fashifashi bila kutoa uchafuzi kwa mazingira.
Kupitia majaribio ya kurudia mara kwa mara, Li na timu yake wameongeza utafiti wa kujitegemea kuhusu ukuaji wa uwezo wa droni wa kujipanga kwenye safu na hali ya usalama katika maonyesho makubwa. Mwaka 2024, timu yake ilifanya maonyesho zaidi ya 50 ya fashifashi za droni ndani na nje ya China, na kushirikiana na maonyesho na majukwaa mengi ya kupiga video fupi mtandaoni katika shughuli za kuendeleza utamaduni.
"Kuhimiza uchumi wa usiku na ule wa anga ya chini, na kutafuta uvumbuzi katika shughuli za kijadi za fataki za fashifashi– ndizo simulizi ninazotamani kuendelea kuandika," Li amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma