Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China laanza mkutano wake wa mwaka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2025
Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China laanza mkutano wake wa mwaka
Mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) ukianza Machi 4, 2025 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine Li Qiang, Zhao Leji, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria kwenye mkutano huo. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING – Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambacho ni chombo kikuu cha mashauriano ya kisiasa cha China, imefanya mkutano wake wa mwaka Jumanne, Machi 4 mjini Beijing, China.

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine walihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa tatu cha Kamati hiyo ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC, uliofunguliwa saa 9 alasiri (kwa saa za Beijing) katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Mkutano huo umepitisha ajenda za mkutano.

Wang Huning, mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China alitoa ripoti ya kazi kwa niaba ya Kamati ya Wajumbe wa Kudumu ya baraza hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha